SNURA MUSHI AINGILIA KATI BIFU LA WEMA, KAJALAhttp://taswirainc.blogspot.com/
MSANII wa filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia
kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na
kuwaagiza wamalize tofauti zao.
Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.

“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,
nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.http://taswirainc.blogspot.com/
0 Response to " "
Post a Comment