Unapokuta Meseji Kama Hii Kwenye Simu ya Mkeo Unafanyaje?


Nilipomaliza chuo kikuu mwaka 2006 niliamua kuanza kutafuta maisha, nilianzia mkoa wa Arusha. Nikapanga chumba katika nyumba iliyokuwa na wapangaji takriban saba. Wakati huo nilikuwa na mchumba na ndoa ilikuwa imekaribia. Nilikuwa nakaa chumba kimoja. Wiki chache kabla sijafunga ndoa, mpangaji mmoja aliondoka, alikuwa anakaa vyumba viwili. Nami nikaenda kwa mwenye nyumba kumwomba nihamie alipotoka yule mpangaji mwingine maana ina chumba na sebule. Nilfanya hivyo kama sehemu ya maandalizi ili baada ya kuoa walau tujibane kwa muda wakati tunatafuta mahali pazuri zaidi (kama mjuavyo kimjini mjini ni jambo la kawaida wanandoa kupanga chumba na sebule, kwa sisi wenye vipato vidogo)

Nilipofika kwa mwenye nyumba, alinikubalia. Wakati ananisindikiza njiani akanipa wosia ambao leo nimeukumbuka maana alichosema ndicho kinachotokea. Kumbuka mchumba wangu huyo alikuwa kaishia kidato cha nne na hakuwa na kazi (house wife). Mzee Mollel aliniambia yafuatayo;
Wanawake ni viumbe wa ajabu sana, chukua tahadhari. Hata kama mkeo ni mzuri sana wa tabia, akishaanza kwenda saloon, kwenye vyama vyao vya kusaidiana, na makundi ya marafiki wenzake (mashoga) ambapo hushinda huko siku nzima, lazima atabadilishwa tabia na kumezeshwa sumu ya tabia mbaya.
Pili, wewe kama mwanaume usihangaike na michepuko, nyama ni ile ile hata kama ukibadili bucha. Tulizana.


Mzee alinitakia kila la heri tukaagana

Mara baada ya kuoa, nilichukua jukumu la kumsomesha mke wangu akarudia sekondari, nikampa msaada wa hali na mali akafaulu, akaenda chuo na sasa ana kazi yake na mshahara wake. Hakika imenigharimu sana laini ndo uanaume wenyewe. Kwa sasa Mungu ametubariki tuna miradi kadhaa, tuna usafiri tuna viwanja, na kimojawapo tunajenga. Nampenda sana mke wangu na huwa napenda awe na vitu vizuri zaidi yangu ili asishawishiwe. Mfano, nimemnunulia simu nzuri sana (smart phone) kuliko zangu, ambapo mimi bado namiliki simu za Tshs 40,000 na Tsh 60,000. yeye ana simu ya Tsh. 300,000. Pia ana biashara zake na wakati mwingine anaenda saloon, na yupo kwenye vikundi vya akina mama wajasiriamali.

Hivi majuzi niliingia chumbani mke wangu akiwa jikoni, nikakuta kaacha simu chumbani, nikaichukua. Nikataka kucheki inbox na whatsapp nikakutana na sms hii;

"Habari ndo hiyo, mpenzi/mume wako akikuambia wewe ni my number one, maana yake ana namba 2, 3, etc. Akikuambia wewe ni special basi jua kuna mitumba, akikuita baby, basi jua anamiliki watu wazima zaidi yako. Akikuita honey basi ujue ana mwingine anamwita Angel"

Nilihamaki kuisoma ile sms, nikaiforward kwangu haraka, nikachukua namba iliyomtumia mke wangu, nikamcheki whatssapp nikakuta ni mwanamke mwenzake. Niliishiwa nguvu, mara nikakumbuka maneno ya Mzee Mollel, ya miaka nane iliyopita.

Mpaka sasa sijui hata nifanyeje na mwenzangu bado hajajua kama nimegundua hilo, japo nataka nimbananishe aniambie logic ya kuwa na msg ya aina hiyo. Najua mwendelezo huu wa kupewa sumu mwishowe atashauriwa achepuke. Nipeni ushauri jamani

0 Response to "Unapokuta Meseji Kama Hii Kwenye Simu ya Mkeo Unafanyaje?"