WIKI iliyopita nilianza kuzungumzia mada hii, lengo ni kukutia moyo. Tambua mafanikio siyo ya wale tu, hata wewe leo hii ukiamua na ukaweka nia, maisha yako lazima yatabadilika.
Hata hivyo, siyo kazi rahisi kama unavyofikiria. Inahitaji mtu mwenye uchungu wa maisha, anayeumia kuwaona watu wenye mafanikio wanavyoyafurahia maisha.
Basi, nimalizie mambo sita yaliyokuwa yamebaki kutimiza yale 15 niliyodhamiria kukupa wewe msomaji wangu.
10. Kushindwa kupo tu
Kufanikiwa siyo rahisi kama baadhi ya watu wanavyofikiria. Ukitaka kuelekea kwenye mafanikio, ujue kuna wakati utakwama. Huna sababu ya kukata tamaa bali kaza mwendo na amini kushindwa ni hatua mojawapo ya kuelekea kule unakotaka.
11. Kukata tamaa ni mwiko
Katika kusaka mafanikio ni lazima utakutana na changamoto nyingi sana. Wapo watakaojitokeza na kusema huwezi kufanikiwa na wengine watadiriki hata kukufanyia fitina.
Hao wasikufanye ukataka tamaa. Yote utakayokutana nayo yachukulie ni safari ya kuelekea kwenye mafanikio kwani njia ya kufika huko haijanyooka. Kuna milima na mabonde hivyo uvumilivu wako utakusaidia wewe kufikia malengo yako.
12. Kujifunza kutoka kwa wengine
Wapo wengi tu ambao wamefanikia. Ukijaribu kuwafuatilia unaweza kukuta kati yao kuna ambao walikuwa maskini kama wewe lakini waliuchukia umaskini na kuutamani utajiri.
Walifanyaje wakafanikiwa? Hilo ndilo la kujiuliza na kama utapata wawili watatu ambao unaweza kuzungumza nao au kusoma habari zao za namna walivyotoka kwenye umaskini hadi kwenye utajiri, itakusaidia wewe kujifunza kitu.
13. Kutoridhika
Hakuna anayeweza kutosheka kwa mafanikio aliyonayo. Ndiyo maana unawaona matajiri wakubwa hapa Tanzania kama Said Bakhresa, Reginald Mengi na wengineo licha ya mafanikio waliyonayo bado wanaendelea kupambana.
Hivyo ndivyo unavyotakiwa kuwa. Usiridhike kwa kila hatua utakayopiga. Ukiwa na milioni moja, jitahidi ziongezeke zifikie mamilioni na hatimaye uingie kwenye orodha ya mabilionea.
14. Kumbuka kusaidia wasiojiweza
Mungu ndiye anayepanga kila kitu. Sisi tunapanga kufanikiwa lakini Mungu naye ana mipango yake.
Aidha, Mungu anawataka wale waliojaaliwa kuwa nacho kuwasaidia wale wasiojiweza. Wale wanaotimiza amri hiyo, huongezewa baraka katika utafutaji wao na ndiyo maana ukifuatilia sana utabaini wale wanaotoa sana ndiyo wanaoingiza zaidi.
Kwa maana hiyo na wewe unapoingia kwenye hatua ya kutafuta mafanikio, usiwe mbahili. Kwa kadiri unavyopata, jitahidi kutoa fungu la kumi kwa wale Wakristo na wale Waislam basi watoe sadaka.
Kiimani hiyo ina nguvu sana katika kuyafikia mafanikio makubwa.
15. Unaweza
Kikubwa ni kuchukua nafasi yako na hakika hakuna kinachoshindikana. Wazungu wanasema; ‘Play your part, it can be done!’ Amini kwamba unaweza kufanikiwa kama wengine.
Ikumbukwe kwamba wengi wanaishi maisha magumu yasiyo na mbele wala nyuma kwa kuwa wanahisi wao wameumbwa waje kuishi hivyo wanavyoishi sasa, siyo sawa!
Wewe ni bilionea mkubwa sana, pambana, fanya kazi kwa bidii na naamini utaondoka hapo ulipo na kwenda kwenye levo nyingine kabisa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI!!!!!!!!!!!!!
0 Response to "MAMBO 15 YA KUZINGATIA KATIKA KUSAKA MAFANIKIO!-TASWIRAINC@BLOGSPOT.COM"
Post a Comment