KOCHA wa zamani wa Everton na sasa Manchester United, David Moyes anaamini kuwa anastahili heshima kutoka kwa mashabiki wa klabu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa ligi kuu hapo kesho uwanja wa Goodison Park.
Mscotishi huyo alizomewa na mashabiki waliosafiri kwenda Old Trafford katika
mchezo wa mzunguko wa kwanza mwezi desemba mwaka jana, lakini bado
anajivunia mafanikio aliyoyapa alipokuwa Goodison Park.
Moyes
aliyeondoka katika klabu hiyo Merseyside mwishoni mwa msimu wa mwaka
jana alizomewa na mashabiki ambao waliona kama amepotea njia.
“Walikuw ana sababu yao ya kunizomea mwezi desemba”.
“Kulitokea matatizo machache pale nilipojaribu kuwasajili wachezaji wao, lakini yote kwa yote nilikuwa nafanya kazi yangu Manchester United”.
“Tulitumia
fedha nyingi kusajili wachezaji nilipokuwa Everton na kuboresha timu,
Nadhani tulijitahidi kwa nguvu zote kuijenga timu hii”.
“Mchezo haunihusu mimi. Ni mechi ya timu mbili zinazohitaji ushindi”.
“Malengo
yao yasiwe juu yangu mimi, waangalie wachezaji wao, lakini najua
mashabiki wa Everton wana haki ya kufanya watakavyo”. Alisema Moyes.
Moyes alitumia pauni milioni 27.5 kumsajili kiungo Marouane Fellaini kutoka Everton katika siku ya mwisho ya usajili.
Pia alikuwa anamtaka beki wa kushoto wa klabu hiyoLeighton Baines.
0 Response to "MOYES AWATAKA MASHABIKI WA EVERTON KUMHESHIMU KESHO soma hapa!!!!!!!!!! TASWIRA!!!!!!!!!!!!!!!!!!"
Post a Comment