Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuacha kuzitumia sikukuu za kidini kwa ulevi, badala yake wajikite kuimarisha upendo na amani.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi alisema hayo
alipozungumzia kuimarishwa kwa ulinzi katika kipindi chote cha
maadhimisho ya Pasaka yanayofanyika katika makanisa mbalimbali.
Msangi alisema kwa kawaida Mkoa wa Mbeya una waumini wengi wa dini,
lakini wapo watu wanaoharibu imani za wenzao kwa kuandaa pombe na
kufanya vurugu wakati wa sikukuu.
“Polisi inawatakiwa kila heri na baraka wakati wote wa
Sikukuu ya Pasaka, lakini lazima tuoe angalizo kuwa wale watakaoshindwa
kujiheshimu kwa sababu ya ulevi watashughulikiwa,” alisema.
Kamanda huyo pia aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuwa makini na
watoto wao watakapokwenda sehemu mbalimbali kufurahia sikukuu. “Tutapita
katika kumbi za starehe kufanya ukaguzi, lengo letu ni kuhakikisha
usalama unakuwepo na watu wanapata nafasi ya kufurahia sikukuu.”
0 Response to "Polisi yawaonya walevi Sikukuu ya Pasaka. | April 20, 2014 | TASWIRA!!!!!!!!!!"
Post a Comment