Taarifa
iliyotolewa asubuhi ya leo na mtoto wa kwanza wa Marehemu Mzee Gurumo
Ndg Abdallah Gurumo amesema kuwa leo saa 10 jioni kutakuwa na kisomo
hapa nyumbani kwa Marehemu eneo la Tabata Kisukulu ambapo Watanzania
wote wanakaribishwa.
Baada
ya kisomo saa 3 ya asubuhi kesho April 15 mwili wa Marehemu utaletwa
nyumbani kwa ajili ya swala kisha saa 4 asubuhi safari ya kuelekea
kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani itaanza kwa ajili ya
maziko ya Mzee Gurumo.
Kwa
mtu usiyepafamu nyumbani kwa Mzee Gurumo ukiwa unatokea Ubungo kabla ya
Mwananchi kuna kituo kinaitwa Garage shukia hapo kisha ulizia mtu
yoyote atakuelekeza pia kwa wewe unaetokea Tabata,Buguruni au Tazara
shukia hapo Garage kituo baada ya Mwananchi.
0 Response to "RATIBA NZIMA YA MAZISHI YA MZEE GURUMO NA SIKU ATAKAYOZIKWA,,,,bofya hapa taswirainc@blogspot.com"
Post a Comment