Ni Dada
yangu wa damu ninayemfata, ana mchumba wake ambaye wamekuwa pamoja kwa
miaka mitatu sasa, wote ni waajiriwa na wanaishi mikoa tofauti. Mwaka
Jana wakakata shauri waoane, mwanaume kafata hatua zote na vikao
vimeanza.
Miaka iyo yote ya mahusiano, kuna msichana ambaye huyo bwana alikuwa anatembea naye japo huyo bwana alikuwa anakana, tena wakati mwingine ananipigia Simu analia nimuombee msamaha kwa Dada yangu, wanamsingizia sio kweli. Basi na mimi namwamini nambembeleza Dada yangu wanasameheana mapenzi yanaendelea.
Sasa hiki kipindi cha sikukuu, akamwambie Dada yangu waende mkoa fulani(sitautaja) wakapumzike sababu wote wapo likizo. Yule bwana katangulia kule Dada naye kafatia, bwana kampokea vizuri hadi hotelini.
Kumbe yule bwana pale hotelini kachukua vyumba viwili( vimefuatana), kimoja kamuweka yule mwanamke ambaye alidai anasingiziwa, kingine kamuweka mke mtarajiwa( Dada yangu) pasipo wao kujua.
Mapumziko yakaisha kila mtu akarudi mkoani kwake, sasa yule mwanamke mwingine kajua ukweli ikabidi amtafute Dadayangu amwambie ukweli, na mbaya zaidi ana ujauzito wa miezi 4. Huyo mdada anadai mwanaume alimwambia wameachana na Dada yangu ndiomana yupo na yeye, na haelewi chochote Kama hata watu wameanza vikao na harusi ipo
karibuni.
Imebidi amwambie mama mkwe wake, mama kampigia mwanae lakini bado anakataa sio kweli, hadi picha katumiwa alizopiga na yule mwanamke anadai zimeeditiwa sio yeye, imebidi mama mtu ampigie muhusika yaani huyo mdada, huyo mdada kakiri kweli na kweli mjamzito.
Wazazi wa mwanaume wamesema hawatambui hilo, binti azae mtoto atachukuliwa, na mipango ya harusi inaendelea, kachanganyikiwa hajui aamue nini, fahamu zinarudi na kupotea tu.

0 Response to " bado siku chache mwanaume ana mwanamke mwingine tena ana ujauzito wa miezi 4 !!!!!!!!!!!!!!!!!!!! TASWIRA"
Post a Comment