Kutokana na ugumu wa maisha wanaume
tumegeuka kuwa walalamikaji linapofika suala la mpenzi wake kuwa very
dependant sana kwako na badala yake tumewageuza na kuanza kuwaita
majina(inferiority complex) kama vicheche,wachunaji,ruba hata muda
mwingine kuwaita Malaya n.k
Na wao kwa kutokufahamu au kutokana na
pressure kutoka kwa wanaume ya kuogopa kusemwa vibaya tumepachikwa
majina na kuanza kuitwa Mabuzi,ATM n.k lakini ukweli wa mambo
ulishawekwa/ulishapangwa bayana na Mkuu wa viumbe vyote,Muumbaji
(Creator),Mwanasheria Mkuu,Mtabiri Mkuu Mwenyezimungu by the way dini
zote uumbaji na mwanzo wa binadamu unatoa maelezo yanayofanana(katika
andishi langu napenda nitumie reference ya biblia)
Mwenyezimungu aliitoa amri hii ukisoma
Biblia GENESIS(MWANZO) aya 3:1-24 hapo ndipo utabiri na utaratibu wa
miasha ya binadamu ,ulipangwa upya mara baada ya Hawa kushawishiwa na
Nyoka(shetani) kula mti wa tunda la katikati naye akamgawia Adam ale pia
, ndipo walipoanza kujua mema na mabaya katika bustani ya Eden
Nanukuu katika aya ya 3 mstari wa 16
GENESIS(mwanzo) 3:16 mwenyezimungu anatoa assignment/task “Akamwambia
mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako,kwa uchungu
utazaa watoto na tamaa yako itakua kwa mumeo,naye atakutawala” -(kumbuka
wenzetu hawajawahi kulalamika hata siku moja kuhusu kusaidiwa
uchungu,kuzaa na tunawatawala they know its NATURE/amri kutoka kwa
Mwenyezimungu)NB;mtawala siku zote ndo mpangaji wa mambo yote refer
serikali katika suala la budget ,budget kama haitoshi/finyu wananchi
watalalamika bila kujua fedha utapata vipi?
Ndipo anapomgeukia Mwanaume na kumpa adhabu/assignment-basic task(ambayo wengi wetu tunalalamika) yake Genesis(mwanzo) 3; 17-19 “akamwambia Adamu kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako ,ukala matunda ya mti ambao
nilikukataza,ardhi imelaaniwa kwa ajili
yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18
michongoma na miiba itakuzalia nawe utakula mboga za kondeni 19;kwa
jasho la uso wako utakula chakula hata utapoirudia ardhi ambayo katika
hiyo ulitwaliwa”
Katika maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa shughuli za ufanikishaji wa kimaisha ya binadamu(MAJUKUMU) katika ngazi ya familia zilishagawanywa(assigned) na Mwenyezimungu katika makundi mawili yaani ya kiuchumi ambayo alikabidhiwa mwanaume so we are responsible to provide Money,rent,shelter ,clothing and other expenses like shopping,Manicures,pedicures Voucher,M-pesa,Tigo-pesa etc na yale ya Uzazi kama kuzaa ,kutunza na kulea watoto wa
familia alikabidhiwa mwanamke
Hivyo basi sio busara na ni kinyume na
mafundisho ya imani ya dini mwanaume kulialia pale your
girlfriend,wife,Mlupo etc anapodai haki yake ya kutunzwa na kukukumbusha
umgharamie kwa sababu wewe ni mtawala wake tena unapaswa utii amri ya
mwenyezimungu ambayo aliitoa Hapo MWANZO 3:1-24 ,Na hata upande wa
UISLAM umeeleza bayana mwanamke akishaolewa hata kama anakazi she isn’t
responsible katika gharama zozote za maisha(hata kuosha vyombo tu) labda
aamue mwenyewe ,jukumu lake yeye ni uzazi na kulea(basic task zile…..)
Nawasilisha tulijadili ,changamoto zinakaribishwa pia
0 Response to "Je Wajua Kuhongwa kwa Mwanamke ni Haki yake Kutoka kwa Mwenyezi Mungu?"
Post a Comment