WATANZANIA WANNE WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA JOMO KENYATTA
Taswirainc@blogspot.com- 2 hours ago

Watanzania wanne (mwanaume mmoja na wanawake watatu) wamekamatwa na kilo
2.2 za heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Watanzania hao waliingia nchini Kenya kupitia Namanga na walikuwa njiani
kuelekea Hong Kong.
"Tumewakamata Watanzania wanne leo (jana) JKIA. Tumewaweka chini ya
uangalizi na tayari wameshatoa vidonge 186 ambavyo tumevifanyia uchunguzi
na kudhibitisha kuwa ni heroin," Ngisa aliliambia Shirika la Habari la
Uchina kwa simu. Ameongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani leo
Ijumaa.
0 Response to "SKENDO YA MADAWA YA KULEVYA JOMO KENYATA"
Post a Comment