Gladness Mallya na Deogratius Mongela
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Katika hali isiyo kawaida denti wa kidato cha kwanza aliyetajwa kwa jina moja la Musa anadaiwa kuwabaka wanafunzi watatu wa shule ya msingi hadi kuwaharibu sehemu za siri.
Tukio hilo la karne lilitokea Kigogo-Luhanga jijini Dar ambapo denti huyo wa sekondari anayeishi na bibi yake aliwabaka watoto hao wanaosoma darasa la kwanza, la pili na la tatu.
Wakizungumza kwa huzuni na kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wazazi wa watoto hao walisema waligundua ukatili huo baada ya kaka wa mtoto mmojawapo kumbana mdogo wake ambapo alieleza jinsi mwanafunzi huyo alivyokuwa akiwafanyia kitendo hicho kwenye banda la kuku wakati watu wamekwenda kwenye shughuli zao.
Akizungumza na Amani, mama wa mtoto mmoja alisema:
“Imeniuma sana, mara nyingi mwanangu anaoga mwenyewe kwa sababu mimi nakuwa kwenye biashara, nakosa muda wa kumkagua ndiyo maana huyu kijana alipata nafasi ya kumharibu kiasi hiki.”
“Bila yule kijana kumshtukia mdogo wake aliyekuwa akitembea kama vile alikuwa ameumia hivyo kupata maumivu, ingetuchukua muda mrefu kubaini kama walifanyiwa kitendo kibaya,” alisema mama huyo.
Mama mwingine ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema, amehuzunishwa sana na kitendo ambacho Musa amewafanyia watoto wao.
Aliongeza kuwa, kwa jinsi alivyo kijana huyo huwezi kudhania anaweza kufanya kitendo cha kinyama kama alichowafanyia watoto wao.
“Kwakweli nikiwa kama mzazi nimeumia sana naomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo isiyofaa kwenye jamii,” alisema mama huyo.
Mzazi mwingine wa kiume ambaye mtoto wake ni miongoni mwa waliobakwa (jina lake tunalihifadhi), amelaani sana kitendo hicho.
“Binafsi kitendo alichokifanya kijana huyo kimenikera mno kwa sababu kitawafanya watoto wetu kutosahau unyama huo katika maisha yao yote,” alisema mzazi huyo.
Watoto hao walikiri kufanyiwa kitendo hicho na Musa kwenye banda la kuku, siku nyingine chumbani kwake.
Wazazi hao walitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kigogo- Luhanga na kupewa jalada la kesi MBL/RB/198/2014, MBL/RB/199/2014 KUBAKA. Mtoto mmoja, mzazi wake alichelewa kwenda kufungua shauri.
Mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni Musa alikuwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi......
0 Response to "DENTI SEKONDARI ABAKA MADENTI 3 WA SHULE YA MSINGI,,,,DA HII NOUMA KWELI!!!!"
Post a Comment