MAKAVU LIVE..!!! KWA WASANII WA MUZIKI NA WAIGIZAJI JUU YA VIDEO CHAFU KATIKA KAZI ZAO...SOMA HAPA

.SOMA HAPA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Malikia wa Bongo Fleva na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed 'Shilole'.
KWENU,Wasanii wa Bongo Fleva. Mnanishangaza sana. Kwa muda mrefu kumekuwa na tatizo la mmomonyoko wa maadili kwa wasanii wa Bongo Muvi. Wamepewa majina yote machafu. Wameonekana ndiyo wavunjifu wakubwa wa maadili. 
Wamekutana na maswali mengi sana huko mitaani; kama wao ni kioo cha jamii, kwa nini wanavaa kihasarahasara? Ni jambo lililoibua maneno sana mitaani.

UNAWEZA SOMA >>> HIZI NDIO MBINU ZA KUMUWEZA, MWANAMKE ALIYE MGUMU KUTONGOZEKA 


Wakati fulani Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity aliwahi kusema, kati ya mambo muhimu atakayoshughulikia katika kipindi cha uongozi wake ni pamoja na nidhamu hasa ya mavazi kwa wasanii wake. 

Hivi karibuni, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba alitoa tamko  kuhusu namna anavyolaani tabia chafu za baadhi ya wasanii wa filamu Bongo. 

Si suala zuri. Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nayo ipo makini sana kuangalia sinema zenye maadili. Sasa mambo yamegeuka. Video za wasanii wa Bongo Fleva zinanuka! 

Imekuwa kama ndiyo sehemu za kujionyeshea miili yao. Huwezi kukaa sebuleni na familia mkaangalia kipindi cha Bongo Fleva kwenye runinga. Ukitaka kufanya hivyo uwe na remote mkononi, maana lolote linaweza kutokea wakati wowote. 

Ni aibu. Hivi, kwani hao mnaowaita Video Queen wakivaa vizuri, nguo zenye heshima, wimbo utaharibika? Aliyewaambia mashabiki wenu wanataka kuangalia maumbile ya wanawake ni nani?




UNAWEZA SOMA >>> ZIJUE SABABU HIZI ZINAZOFANYA WANAWAKE WAVAE NUSU UCHI 

Hayo mambo si yetu. Mmeiga staili ya muziki kutoka nje, sawa! Na mavazi pia? Na uhuni wao? Hapana.
 Ngoja niwape mfano mmoja; tusiende mbali sana, angalieni mfano mzuri kutoka hapo Afrika Kusini.

Mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Lady Jaydee.


Wanapiga Kwaito safi kiasi kwamba kuna wasanii wengine wameanza kuiga, lakini angalia mavazi yao. Mmewahi kuwaona wakicheza uchi? Hakuna kitu kama hicho. 

Huu utamaduni tunaupata wapi? Kumbuka ni kichaa tu ndiye anayeweza kupita barabarani akiwa mtupu. Sasa kama ninyi mna akili timamu, mnawezaje kujiachia utupu kwenye video ambazo zitaonekana na wengi? 

UNAWEZA SOMA >>> MAMBO 11 AMBAYO MWANAUME ANATAKIWA KUYAFANYA ILI KUMRIDHISHA MWANAMKE NA KUJIHAKIKISHIA KUMMILIKI KABISA !!! 

Au hamna wazazi? Hamna ndugu wanaowaheshimu? Hamna watoto? Kwa nini mnajidhalilisha? Jambo la kushangaza zaidi, wasanii wengi nimewasikia wakihojiwa na vituo mbalimbali vya runinga na redio, wanalalamikia kuzuiwa video zenye uchafu! 

Eti wanasema, wanataka soko la kimataifa. Kama kweli ili kuwa wa kimataifa ni lazima ujianike utupu, kuna faida gani? Si bora mnabaki kuwa wasanii wa Tanzania tu? 

Wapo baadhi ya wasanii wameamua kuachia video zao online wakijua kuwa ni chafu; hapo ni sawa na kukimbia vivuli vyao wenyewe! Hata hivyo si wote wenye tabia hizo, wapo baadhi wanaotoa video zenye maadili safi kabisa ya Mtanzania – mfano mzuri ni Historia wa Lady Jaydee na wengineo. 

UNAWEZA SOMA >>>> ZIJUE FAIDA 17 ZA KUJAMIIANA. SOMA HAPA 
Ninyi mnapaswa kuwabadilisha wenzenu malimbukeni, mtazamo wa fikra. Sitafunga domo langu ng’o!   Yuleyule, Mkweli daima,  
Joseph Shaluwa    



0 Response to "MAKAVU LIVE..!!! KWA WASANII WA MUZIKI NA WAIGIZAJI JUU YA VIDEO CHAFU KATIKA KAZI ZAO...SOMA HAPA "