Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametishia kuwafukuza kutoka nchini humo
wanadiplomasia wanaopigia debe mapenzi ya jinsia moja. Katika hotuba
yake ya sherehe za kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo, Mugabe alitumia fursa
hiyo, kukaripia kile alichokiita upuuzi wa nchi za ulaya zinazohubiri
ushoga Alituhumu nchi za ulaya kwa kukosa maadili na kusisitiza kuwa ndoa inaweza kuwa tu kati ya mwanamke na mwanamume.
Sio mara ya kwanza Mugabe amekemea swala la ushoga.
Aliwahi kuwataja mashoga kuwa wabaya kuliko Mbwa na Nguruwe.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Zimbabwe na mashoga hukamatwa mara kwa mara kwa kosa hilo.
|
0 Response to "Saturday, April 19, 2014 Mugabe awakemea mabalozi kuhusu ushoga soma hapa!!!!!!!!! TASWIRA!!@!!@!!@!!!!!!!!!!!@"
Post a Comment