taswira
Na Shakoor Jongo
DIVA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amechukizwa na kitendo kilichofanywa na staa mwenzake katika tasnia hiyo, Jacqueline Wolper Massawe cha kukacha kumzika msanii mwenzao Steven Charles Kanumba na kwenda kwenye shughuli binafsi nchini Malaysia, Risasi Jumamosi linakumegea kwa kirefu zaidi.
Uwoya aliliambia gazeti hili mara baada ya maziko ya Kanumba kuwa kitendo hicho kimemchefua na ameapa kwamba akikutana na Wolper lazima ampe kichapo cha nguvu.
SABABU TATU
Uwoya alizitaja sababu tatu zilizokuwa zilizomfanya Wolper kutokumzika Kanumba aliyefariki Aprili 7, mwaka huu na kuzikwa Aprili 10 kuwa ni;
UNAFIKI
Uwoya alisema sababu ya kwanza iliyokuwa ikimtaka Wolper kusitisha safari yake hiyo ni unafiki kwa kuwa msanii huyo siku ya kwanza ya msiba nyumbani kwa marehemu Kanumaba alilia hadi kuzimia na siku ya pili alikwea pipa na kutimkia nje ya nchi.
“Haiwezekani leo uonekane ukilia hadi kuzimika kisha kesho yake uondoke na kwenda kwenye shughuli zako, kama huo si unafiki unaweza kuuita ni kitu gani?” Alihoji Uwoya.
cheo chake bongo movie
Uwoya alisema kuwa Wolper ana cheo ndani ya klabu yao ya Bongo Movie ambacho kilikuwa kikimtaka kuwepo msibani kuanzia mwanzo hadi mwisho hata kama alikuwa na dharura ya kiasi gani.
“Sijui ataonekanaje mbele ya viongozi na wanachama wa Bongo Movie ambao ndiyo waliompa cheo hicho, kwa maana nyingine atakuwa haaminiki pindi siku nyingine litakapotokea tatizo, ingekuwa vyema akavuliwa cheo hicho,” alisisitiza Uwoya.
ALISHAWAHI KUTOKA NA KANUMBA
“Tuachane na yote, kitu kikubwa zaidi Wolper alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba, huyo ndiye mtu aliyemfanya awe staa na jamii imtambue kwa nini anaacha kumzika na kwenda kufanya mambo yake binafsi?” Alihoji kwa hasira.
Uwoya aliendelea kumponda Wolper kwa kusema kuwa hakuwa muungwana wa kuweza kulipa fadhila kwa Kanumba ambaye amemsaidia kumfanya jamii imtambue.
Hata hivyo, Uwoya ambaye sasa anafahamika kama mama Dagraei Krish, alimmwagia sifa mwigizaji mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kitendo chake cha kuwaamrisha wafanyakazi wake kufunga ‘pub’ yake kuonesha kuwa ameguswa na kifo cha Kanumba.
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini wamemuunga mkono Uwoya kutokana na mtazamo wake huo kuhusu Wolper.
Wolper alikwea ‘pipa’ Aprili 8, mwaka huu kutimkia Malaysia kwenye shughuli zake binafsi na kushindwa kumzika Kanumba ‘The Great’.

0 Response to "UWOYA,ASEMA LAZIMA NIMPIGE WOLPER....PATA STORY ZAID HAPA CHINI TASWIRAINC@BLOGSPOT.COM"
Post a Comment